Monday, November 7, 2011

Mandhari ya Ziwa Nzerekela - Selous Game Reserve

Ziwa Nzerekela linavyoonekana ukiwa unalikaribi kutokea moja ya barabara ndani ay pori la akiba la Selous. Ni Moja ya maziwa makubwa ndani ya pori la akiba la Selous.


Ziwa hili ni kubwa kiasi cha kuwa na visiwa kadhaa ndani yake. Nilidokezwa ya kwamba kwa wale wanaopenda kuangalia ndege mbalimbali, visiwa hivi huwa na ndege wengi ambao huenda huko kupata hifadhi na kuzaliana. Hali ya kisiwa inawakwamisha wanyama wakubwa wa ardhini ambao huharibu mayai na kudhuru au hata kula watoto wa ndege hao.

Ukubwa wa eneo na kina cha maji kuwa cha kutosha ni sababu tosha ya kufanya baadhi ya kampuni (zenye vibali) kuendesha boat safari ndani ya ziwa hili. Kibali kinahitajikwa kwa boat safaris ambazo zinafanyiwa ndani ya pori la akiba la Selous. Campsite kadhaa zilizopo ndani ya pori la akiba ndio zimeruhusiwa kuendesha safari za boat ktk Ziwa Nzerekela au Manze. Picha juu ni Boat ambayo inaamika kuwa inamilikiwa na Impala camp ikifanya safari na wageni ndani ya ziwa Nzerekela

No comments:

Post a Comment