Tuesday, October 4, 2011

Ni safari ya Kuelekea Uhuru Point - Mt Kilimanjaro

Ilikuwa ni safari ambayo ilisimamiwa na Kampuni ya Tanzania Travel Company. Safari iliyopitia route ya Machame. Kwa kawaida safari ya kupitia route ya Machame huchukua siku sita mpaka saba (kupanda na kushuka). Tofauti iliyopo kwa ruote hii na ile ya Marangu ni kwamba malazi ktk route ya Machame ni mwendo wa tented camping. Tofauti na ile ya Marangu ambako wageni wanakuwa na vyumba vya kulala katika vituo maalum - huts. picha juu ni kundi la wageni likiwa eneo la Baranco likijiandaa kuchapa mwendo kuelekea mbele. Ni moja ya njia ambazo zinafaa kwa wale ambao wanapenda kupanda mlima taratibu ili kuuruhusu mwili kufanya acclimatization vyema.

What a birthday celebration.... Kijana huyu alitimiza miaka 21 akiwa safarini kuelekea Uhuru point. Wenyeji wake baada ya kubaini hilo walifanya ubunifu na kumpa birthday cake ya aina yake. Truly creative... (picha zote kwa hisani ya mdau Sam Diah wa Tanzania Travel Company)

No comments:

Post a Comment