Wednesday, October 19, 2011

Mv Liemba ileee.....

Mv Liemba ni Moja ya Meli kongwe Duniani ambayo inafanya safari zake ndani ya Ziwa Tanganyika. Inaelezwa ya kwamba meli hii ilitengenezwa Mwaka 1927 na bado inapiga mzigo mpaka sasa. Inafanya safari zake kati ya Miji ya Kigoma kwa Tanzania na Mpulungu upande wa Zambia.
Picha hizi zilipigwa na wadau wa Kima Safaris waliokuwa mapumzikoni ktk hoteli ya Lake Shore Lodge huko mkoani Rukwa pembezoni mwa Ziwa Tanganyika.

Kwa mwelekeo wa meli hapo ilikuwa kwenye safari yake ya kwenda Zambia.

Bofya hapa kujua dondoo zaidi kuhusu Meli hii - misukosuko na mabadiliko iliyofanyiwa mpaka kufika hapo ili sasa. Ni Sehemu ya historia ya Utawala wa Wajerumani ktk Africa, hali inayoifanya meli hii kuwa kivutio cha utalii kwa wale wanaopenda kufuatilia mambo ya kale.

No comments:

Post a Comment