Friday, October 28, 2011

Lake Tanganyika tokea Hewani...

Lake Shore lodge & Campsite ina uwanja mdogo wa ndege unaowezesha wageni kufika na kuondoka kwa ndege ndogo. Picha juu ni ndege ndogo ilikuwa imekwenda hapo kuwachukua wadau wa Kima Safaris waliokuwa mapumzikoni huko. Mtundiko huu unakuletea taswira mbalimbali za maeneo pembezoni ya ziwa Tanganyika tokea angani.

Huu ni muonekano wa ziwa Tanganyika mita chache tu baada ya ndege kuagana na ardhi. Kwa wale wanaotafuta 'beach' plots ni dhahiri ufukwe wa ziwa Tanganyika bado upo wazi kwa wageni. Sehemu kubwa bado ni wazi sio kama pwani ya bahari Hindi.

Ni Baadhi ya Visiwa vilivyopo ndani ya ziwa Tanganyika eneo la Kipili mkoani Rukwa.


Pwani bado haijachakachuliwa - so natural...

Mita kadhaa baada ya kuachana na ukanda wa pwani ya ziwa Tanganyika unakutana na msitu asilia kwa kwenda mbele. [Taswira - Kim Safaris Ltd]

1 comment:

  1. Tatizo ninaloliona katika hii habari ya watu kuchukua na kumiliki maeneo ya ufukweni ni kwamba kabla ya hapo, wenyeji wanatumia maeneo hayo kwa uhuru kamili. Wanavua, wanaogelea, wanatembea katika maeneo hayo. Lakini akija mtu kununua na kufungia uwigo, hakuna tena uhuru huu kwa wenyeji. Sioni kama ni busara hata kidogo.

    Badala yake, napendekeza kuwa wanaonunua maeneo hayo wasiruhusiwe kununua hadi ufukwe. Waishie mbali kidogo, labda mita hamsini kutoka linapoanzia Ziwa, ili wavuvi na wengine wanaotumia ufukwe wasizuiwe uhuru wao.

    Nasema hivi kutokana na niliyoyaona Ukerewe, ambapo sehemu ambazo wenyeji walikuwa wakitumia kwa kuoga na kadhalika zimechukuliwa na wawekezaji. Inasikitisha jinsi jadi ya watu ya karne na karne imefifishwa ghafla.

    ReplyDelete