Wazee wa porini walipoamua kuwapa majina ya wa juu na wa chini, chui na duma walikuwa hawajakosea. unaweza kutetereka kubaini nani ni nani kutokana na kushabihiana kwa mabaka ya ngozi zao. tabia zao baada ya mawindo ni moja ya mambo ambayo huwatofautisha wazi wazi. Wa juu (chui) huwa na tabia ya kupandisha windo lake juu ya mti na huko ndipo hukaa na kula windo lake. Hufanya hivi ili kukwepa ushindani baina yake na wajanja wengine kama Simba au wazee wa mizoga aka bwana afya. picha juu ni swala ambae alikuwa keshauwawa na wajuu. Wajuu aliyemtundika hapo alitokomea baada ya kuona wageni wake wakimsogelea
Huyu ni wa chini (Duma),, yeye huwinda na kumaliza shughuli yote chini. Wa chini haja ujanja wa kukwea mti yeye mwenyewe, achilia mbali kupandisha windo lake. Hapa alikuwa akivuta pumzi baada ya kumaliza kimbembe cha kumkibiza swala huyu. Picha Mdau Tom wa Kima Safaris
No comments:
Post a Comment