Tuesday, August 2, 2011

Marangu Route - Mlima Kilimanjaro

Umbali toka Geti la Marangu mpaka Uhuru point ni Kilometa 36.5. hii inamaanisha kwa safari yote (kupanda na kushuka) mgeni hutembea umbali usiopungua Kilometa 73.

Route ya Marangu pia huchukuliwa na wengi kama njia 'nyepesi' ya kukwea mlima Kilimanjaro Hali ambayo imepelekea wengine kuibatiza jina la Coca-cola route (wakiifananisha na kinywaji 'cha watoto'). Ruti ya Machame ambayo inaelezwa na wengi kuwa yenye changamoto nyingi imepewa jina la Whiskey route.

Dhana ya kwamba njia ya Marangu ni njia rahisi huwavutia wapandaji ambao wanakuwa hawajajiandaa vyema kuichagua njia hii ktk kutimiza azma yao ya kuukwea mlima Kili. Hali hii imepelekea idadi ya wapandaji wanaoshindwa kufika juu kileleni kwa njia ya Marangu kuwa wengi ukilinganishwa na njia za wagumu ambako wapandaji wengi huwa wanakuwa wamejiaanda kwa shuluba za mlima. Kimsingi, kupanda mlima Kilimanjaro ni jambo ambalo linahitaji maandalizi mazuri kwa mpandaji kabla hajaanza safari. Mazoezi ni namna nzuri ya kuuandaa mwili kwa kupanda mlima. Kuzingatia masharti na taratibu za upandaji ni moja ya vitu vya kuzingatia wakati wa kupanda ili uweze kufika Kileleni.

Picha zote mbili ni huts za kufikia wageni zilizopo Mandara hut. Hii ni point ya kwanza kabisa baada ya kutoka Marangu geti ktk njia ya Marangu. Ipo umbali wa Kilometa 8.3 tokea geti la Marangu - unapoanzia safari.
(picha - Maktaba ya TembeaTz)

No comments:

Post a Comment