Monday, July 25, 2011

Ziwa Duluti - Arusha

Ziwa Duluti ni moja ya Maziwa ambayo yapo ktk lile kundi la "hawavumi lakini wamo.." Ni Ziwa ambalo lipo mkoani Arusha, pembezoni mwa barabara kuu ya Moshi-Arusha. takriban kilometa 5 Toka barabara kuu eneo la Tengeru.

Ziwa hili limo ndani ya eneo tengwa la Msitu wa Duluti. Ni Eneo ambalo linasimamiwa na idara ya misitu. Kimsingi, ziwa hili limezungukwa na msitu wa Duluti kila upande hali ambayo inatoa mandhari nzuri kwa mgeni anayelitembelea. Wageni wanaolitembelea ziwa (na kuingia eneo tengwa) hulazimika kulipa kiingilio

Eneo linalolizunguka Ziwa hili lina wanyama wadogo wadogo kama Dikidiki, Swala, Tumbili na aina nyingine za Ngedere pamoja na Kima. Sambamba na hao ziwa hili lina umaarufu wa kuwa na kenge wakubwa tu.. Kwa yule mpenzi wa kuangalia aina za ndege mbalimbali, Lake Duluti patamsuuza roho yake. Mchanganyiko wa Ziwa na Msitu umepelekea kuwepo na ndege wengi sana eneo la Ziwa Duluti. Wapo ndege ambao wamepafanya hapa ni makazi yao na wapo ambao huwa wanapita wanapokuwa kwenye safari zao - migratory birds. Hapa utakutana na ndege kedekede ambao huishi majini au kutegemea uwepo wa maji kwa ajili ya kujipatia chakula. Eneo hili halina wanyama wakubwa tunaowazoea kuwaona kwenye hifadhi za taifa ukiachia ndege na hao wadogo wadogo niliowataja.

Ni Sehemu yenye utulivu wa kipekee. Pembezoni mwa ziwa hili pia kuna Hoteli ya Lake Duluti Lodge ambayo wageni kadha wa kadha hufika kwa mapumziko

Mandhari Mwanana
Shukran ya picha kwa Mdau Francis wa Lake Duluti Lodge

No comments:

Post a Comment