Monday, July 11, 2011

Upekee wa Ngorongoro

Ngorongoro crater ni moja ya vivutio ambavyo vinapatikana ndani ya eneo la hifadhi la Ngorongoro yaani Ngorongoro conservation area authority (NCAA). vivutio vingine ni crater ya empakaai.
Moja ya mambo yanayolifanya eneo la NCAA kuwa na upekee ni uhifadhi ambao unawaweka pamoja wanyama pori pamoja na wanadamu (Wamaasai). Mara nyingi ktk maeneo ya uhifadhi, wananchi huondolewa na kuwapisha wanyama na maliasili nyingine zinazopatikana eneo husika. Kwa Ngorongoro crater, Ushahidi wa haya unkutana nao ukiwa nje ya ngorongoro crater (lakini ndani ya eneo la NCAA). Usije kustaajabika kwa kuona Ngombe, Kondoo, punda sambamba na Wamaasai wakiwa sambamba nao.

Watoto nao wanakuwepo pembezoni mwa barabara hii. hii ni barabara iliyo nje ya crater (crater rim) ambayo ndio hiyohiyo itakayokufikisha hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Upande mwingine wamaasai wameruhusiwa kujenga makazi na kuishi ndani ya eneo.

Mbuzi wakiwa malishoni pembezoni mwa barabara.

Ujasiriamali upo pia umasaini. Hawa huuza vitu mbalimbali ambavyo wanavitengeneza kwa mikono.
(Picha - Mdau GBM)

No comments:

Post a Comment