Tuesday, June 14, 2011

Mageti ya kuingilia Ngorongoro (NCAA)

Hili ndio geti kuu la kuingilia Ngorongoro Conservation Area, eneo ambalo linasimamiwa na Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA). Unakutana nalo ukiwa unatokea Karatu. Hivi ndivyo lilivyo sasa baada ya kupigwa soap-soap mwaka 2009/2010. Geti hili linafahamika kama geti la Lodware.

Kuna sehemu ya kupata taarifa mbalimbali zinazohusu
Ngorongoro Conservation Area Authority.

hili ni geti la kushukia Crater. Geti hili linatumika kwa kushukia tu - descent. Wale wanaomaliza mizunguko yao wanatokea kwenye geti jingine. Geti hili linafahamika sana kama descent gate lakini jina lake ni geti la Seneto. Lile la kupandia (kutokea crater - ascent) linajulikana kama geti la Lerai. Baada ya saa kumi Jioni hakuna mgeni anayeruhusiwa kushuka crater. Hotel zote za Ngorongoro na camp site za wageni zipo nje ya crater.

Mnapoingia Ngorongoro (ukiwa unatokea Arusha), utakutana kwanza na geti la Lodware (picha ya kwanza). Hilo geti linatumika kwa wale wanaoingia shimoni (crater) na hata wale wanaopitiliza kuelekea Serengeti au Musoma.
Kwa yule ambae safari yake inaishia Ngorongoro crater na ana mpango wa kuingia crater, basi itamlazimu kulipa gharama za kuingia ndani ya NCAA ambapo kichwa ni Sh 1000 na gari Tsh 10,000 (kutegemea na uwezo wa gari). Atapewa risiti pale lodware ambayo atalazimikiwa kuionyesha akifika geti la Seneto anapotaka kuingia shimoni kwenyewe. gharama za Ngorongoro hazijalishi kama wewe unapita (kuelekea Serengeti au Musoma) au unaingia shimoni kwa matembezi.
Kwa yule ambae anapita NCAA kuelekea Serengeti au Musoma, atalipa gharama za kupita Ngorongoro (NCAA) - Transit - na atakapofika geti la Naabi Hill (Serengeti) atalazimika kufanya malipo kwa ajili ya kuingia hifadhi ya taifa ya Serengeti. Upande wa Serengeti gharama zinakuwa 10,000 (gari ilisyosajiliwa TZ) na 1500 kwa kichwa (raia wa EA).
(picha | Mdau GBM hivi kribuni)

1 comment:

  1. Thanks for the facts. Posts zako zinajieleza vyema kaka. Keep up the good work

    ReplyDelete