Wednesday, May 11, 2011

Taswira Maridhawa za Maundi Crater - Mt Kilimanjaro

Ukifika Maundi crater unakaribishwa na hicho kibao. crater yenyewe ipo nyuma ya hicho kibao. kwa siku ambazo hakuna mvua au mawingu, ukiwa Maundi crater unaweza kuona mji wa Moshi na pia kuiona +254.


Njia inayoteremka na kukuingiza ndani ya crater kabisa. ruxa kwa mgeni kuingia na kujionea mandhari mpaka ndani ya crater.

Sehemu kubwa ya mzunguko wa juu wa crater - crater rim, imezungukwa na miti

Kwa yule atakae penda kufanya Day trip kupitia Marangu route, Maundi crater (akiwa na nguvu) ndio mwisho wa kibali chake/safari yake. hapa unaweza ukakaa muda unavyokuruhusu. licha ya kwamba hapa ni sehemu mwanana kupumzikia, si ruhusa kupata maakuli muwapo hapa. shughuli zote za msosi zinafanyika Mandara hut au maeneo maalum kwa ajili ya chakula muwapo safarini.

No comments:

Post a Comment