Wednesday, May 4, 2011

Taswira Maridhawa - Tarangire

Kundi hili la pundamilia tulilikuta pembezoni mwa moja ya mabwawa ya maji ndani ya hifadhi ya taifa ya Tarangire. Bwawa hili lipo pembezoni mwa barabara inayozunguka ndani ya hifadhi.
Hawa walikuwa upande wa pili wa barabara wakisubiri tupite ili nao waweze kuvuka na kuja kunywa maji.

(Picha | Maktaba ya TembeaTz)

No comments:

Post a Comment