Friday, April 29, 2011

Game Ranger - Tarangire

Unapofanya safari ya miguu ndani ya hifadhi au pori la akiba (Game walking Safari) ni lazima mgeni asindikizwe na Askari wa wanyama pori na tena mwenye silaha. Ni utaratibu ambao una manufaa mengi kwa mgeni. Awali mgeni anakuwa na uhakika wa kuongozwa njia na mtu mwenyeji - mwenye kuelewa njia za kupita na kufika mahali panapotakiwa. ukiachia hilo, askari hawa wamepewa mafunzo ya kuweza kutambua hali na tabia za wanyama. hii huwapa uwezo wa kuwakwepesha wageni dhidi ya wanyama hatari kabla hatari haijatokea. Mathalan, mbogo aliye peke yake ni hatari kushinda mbogo walio kwenye kundi. Ranger mmoja hutakiwa kusimamia si zaidi ya wageni 5. mkizidi, inabidi muongeze ranger mwingine.

Kitu kingine ni uelewa na maarifa waliyonayo askari hawa ambayo wanakuwa wanakuelimisha muwapo safari. safari za miguu ni moja ya aina ya Safari ambayo itakukutanisha na mtu ambaye eneo la hifadhi ndio nyumbani kwake. Ukiwa mdadisi na mtu wa kupenda kujua, utatoka na uelewa mkubwa wa mambo mbalimbali ya porini - wanyama na mazingira yao.

Maisha ya hawa askari nayo ni ya namna ya kipekee. Kuna kipindi wanakuwa doria kwa kipindi cha zaidi ya wiki 2 porini bila kurudi makwao. Wanaishi kwa kupiga kambi ktk vituo vyao vilivyopo ndani ya hifadhi kipindi chote. Lengo kuu likiwa ni kuhakikisha ustawi endelevu wa hifadhi zetu za taifa. huko hupambana na changamoto nyingi zenye kusisimua na kusikitisha pia.

Pichani ni Ranger aliyeniongoza nilipofanywa Game walking safari ndani ya hifadhi ya Tarangire mwaka jana.

No comments:

Post a Comment