Thursday, March 3, 2011

Taswira moja huleta nyingine

Wakati tumemaliza mizunguko ndani ya hifadhi na kufika palipo geti la kutoka nje ya hifadhi ya Tarangire, nilivutiwa na muonekano wa huo mti na kuamua kuupiga picha. Mti huu upo nyuma ya majengo ya kufanyia malipo na ukaguzi getini hapo. Nilipokuwa naanza, lengo lilikuwa ni kunasa taswira ya huo mtu. Wakati nikizoom mti huu, niligundua uwepo wa kitu kingine ambacho nacho kilinivutia japo kilikuwa mbali kidogo na nilipo.

Lilikuwa ni kundi la Temba aka Masikio kadhaa ambao walikuwa wanakula karibu na eneo la getini. Baada ya kunasa taswira ya mti, nilianza kunasa taswira za tembo hao ambao mkao wao na mazingira waliyokuwamo vilinivutia ki-ukweli.


Lilikuwa ni kundi lenye mchanganyiko wa wakubwa na watoto. Kimsingi, kundi la tembo lenye watoto si la kulikaribia. mama tembo hulinda watoto wao kwa nguvu zote. uwepo wako karibu nao unaweza kuwa na madhara. hapo sijazungumzia hatari ya kumpiga picha kwa flash, hii ni hatari nyingine ya kuikwepa unapokuwa karibu nao.

(Picha | Maktaba ya TembeTz)

1 comment: