Thursday, March 3, 2011

KUKARIBISHA MAOMBI YA VITALU VYA UWINDAJI WA KITALII

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

TANGAZO MAALUM

KUKARIBISHA MAOMBI YA VITALU VYA UWINDAJI WA KITALII KATIKA KIPINDI CHA UWINDAJI CHA MWAKA 2013 HADI 2018

(Limetengenezwa chini ya Kifungu cha 9(2) cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori, Sura ya 283 (Kanuni za Uwindaji wa Kitalii za mwaka 2010)

Wizara ya Maliasili na Utalii inakaribisha maombi kutoka kwa kampuni zenye sifa zinazohitaji kugaiwa vitalu kwa ajili ya kuendesha biashara ya uwindaji wa kitalii kwa kipindi cha kuanzia Julai, 2013 hadi Machi, 2018. Jumla ya vitalu 156 vimetengwa kwa ajili ya ugawaji kwenye mapori ya akiba (Game Reserves), mapori tengefu (Game Controlled Areas) na maeneo ya wazi yenye wanyamapori (Open Areas). Vitalu hivyo vimepangwa katika makundi matano kulingana na ubora (Kiambatisho). Kampuni ya uwindaji wa kitalii inaweza kugawiwa hadi vitalu vitano (5) ambavyo vitakuwa katika makundi mchanganyiko ya ubora.

1. SIFA NA TARATIBU ZA KUOMBA KITALU CHA UWINDAJI

Kulingana na matakwa ya Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori, Sura ya 283, ugawaji wa vitalu utafanyika baada ya waombaji wenye sifa kutuma maombi na kukubalika. Mwombaji wa vitalu anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

(a) kuwa na kampuni iliyosajiliwa na Msajili wa Kampuni Tanzania kwa ajili ya uwindaji wa wanyamapori;

(b) uzoefu wa angalau mmoja wa wakurugenzi usipungue miaka mitano katika fani ya biashara na uhifadhi wa wanyamapori nchini; na

(c) kwa kampuni za ubia kati ya Mtanzania na wageni, hisa za Mtanzania zisipungue asilimia ishirini na tano ya hisa zote zilizolipiwa (Subscribed shares).
[Soma zaidi...]

No comments:

Post a Comment