Saturday, March 12, 2011

Serengeti Balloon SafariKivuli unachokiona kwenye nyasi ni kivuli cha balloon tuliyokuwamo. Hapa tulimuomba Rubani wa Balloon letu alipeleke juu ili tuweze kuona uwanda wa Serengeti toka kwa juu. The view was breathtaking...

Safari za Balloon ndani ya hifadhi ya taifa ya serengeti zinaendeshwa na kampuni ya Serengeti Balloon safaris. Njia nzuri na rahisi ya kuweza kupata booking ya balloon flight ni kwa kupitia tour operators.

Safari hizi huanza alfajiri (yetu ilianza saa 12 asubuhi) kabla jua halijachomoza. Awali tuliamshwa hotelini (serena Serengeti) saa kumi usiku na kupewa kifungua kinywa kabla ya kuanza safari ya kuelekea Maasai Kopjes ambako ndio kuna launch site ya Balloon. Ni vyema kuijulisha hotel uliyofikia kuwa kesho yake upo ktk mpango wa balloon flight ili waweze kukuamsha mapema na kukuandalia staftahi. kwa wageni wanaofikia hotels/campsites zilizopo maeneo ya Central serengeti, Kampuni ya Serengeti Balloon safaris ina wawakilishi wake ktk hizo hotels na wao ndio watakaokuchukua asubuhi na kukupeleka sehemu ya kurushia Balloon . Muda wa kuondoka hotelini kwenda Launch site unategemeana na umbali kati ya sehemu ya kurukia Balloon na hotel/campsite uliyofikia. Kwa kawaida wageni au magari yasio ya wanahifadhi hayaruhusiwi kutembea ndani ya eneo la hifadhi baada ya saa 12 jioni (giza likiingia). Kampuni ya Serengeti ballon Safaris wao wana kibali maalum kinachowawezesha kutumia magari yao mida yote ili kuweza kuratibu shughuli zao. Kwa namna nyingine safari ya kutoka hotelini kwenda Maasai Kopjes huwa ni kama night game drive. Tukiwa njiani tulikutana na fisi wakiwa bize kupita maelezo, mmoja alipita karibu na gari yetu na kutoa kicheko. Sehemu nyingine tulikutana na kiboko aliyekuwa nje ya bwawa ktk mto Seronera. Alikuwa ni mkubwa ki ukweli..

Muda wa flight unategemea na hali ya upepo, kwani hizi balloons zina sehemu maalum za kutulia hivyo upepo ukiwawahisha kufika landing site itawalazimu mtue. lakini mara nyingi safari huwa si chini ya saa moja. Yetu ilichukua takriban saa moja na robo na tulisafiri kama 18kms hivi. Baada ya flight ni mwendo wa bush breakfast chini ya mti.

Yawezekana maelezo haya nilishawahi kuyatoa hapo awali lakini leo nimeona ni vyema niyarudie baada ya kukutana na mdau mmoja leo mchana aliyeonyesha hamasa ya kutaka kujua utaratibu na jinsi ya kufanya ballon flight. natumai wengi mtakuwa mmenufaika. Kwa taarifa tu, hivi sasa Balloon flights zipo pia hifadhi ya Taifa ya Tarangire. Usisite kudadisi zaidi kwa kuuliza swali kupitia tembeatz@gmail.com Tutajitahidi kutoa ufafanuzi kadri iwezekanavyo.

No comments:

Post a Comment