Wednesday, January 12, 2011

Wajumbe wa bodi na walimu wa shule ya St Anthony walipotembelea Kisiwa cha Mbudya

Tarehe 11.01.11 Baadhi ya wajumbe bodi na walimu ya shule ya Mt. Anthony ya Mbagala DSM walifanya safari na kutembelea kisiwa cha Mbudya kilichopo ktk pwani ya Dar. safari ilianzia Belinda Beach ambapo ndipo wageni hao walipanda boat na kuelekea ktk kisiwa cha Mbudya.

Moja ya boti iliyowabeba wageni kuelekea kisiwani ikiwa safarini.

Boti nyingine iliyokuwa imebeba wageni wengine ikiwa inakaribia kutia nanga ktk kisiwa cha Mbudya
Boti ya kwanza iliyobeba baadhi ya wageni ikiwasili ktk Kisiwa cha Mbudya

Boti nyingine nayo ikiwa imefika ukingoni mwa bahari ktk kisiwa cha Mbudya


Awali kulikuwa na mazungumzo mafupi ya kutakiana heri na fanaka ya kuuona mwaka mpya wa 2011.

Kikundi cha Super Kamambe dance kilikuwepo kisiwani ili kutoa burudani ya ngoma mbalimbali za Asili. Safari hii ilikuwa chini ya usimamizi wa Kampuni ya Pongo Safaris

1 comment: