Thursday, December 9, 2010

Mwananyika - Kijiji cha Mloka (Selous GR)

Huyu jamaa anafahamika sana kama Mwananyika ambae hupatikana ktk kijiji cha Mloka, hujishughulisha na shughuli ya kuwatembeza watalii ktk maeneo ya kijiji cha mloka na kuwaonyesha utamaduni wa wanajamii ya kijiji hicho. Anapokuwa na wageni huwatumbuiza kwa nyimbo anazoimba huku yeye mwenyewe akiongoza kuzicheza.

Katika matembezi, wageni hupata fursa ya kupitishwa ktk vichaka vilivyopo na kuonyeshwa miti mbalimbali ambayo jamii ya kijiji hiki hutumia kwa shughuli mbalimbali ikiwemo dawa.

Hapa akiwa kamaliza safari na kuwarudisha wageni ktk camp ya Hippo iliyopo pembezoni mwa mto Rufiji (unaonekana kwenye background). Kijiji cha Mloka kipo nje kidogo ya pori la akiba la Selous na ni kijiji ambacho kuna kambi kadhaa za kufikia wageni (ambazo zipo nje ya hifadhi). Ahsante ya picha kwa Mdau Tom wa Kimasafaris

1 comment:

  1. Nafikiri sio utamaduni tu, bali pia ni sehemu ya ajira aka kujipatia kipato.

    ReplyDelete