Monday, November 15, 2010

"Rainbow" iliyolizunguka jua leo Dar

Kwa wali tuliokuwa Dar leo (sina uhakika na maeneo mengine nchini na Duniani), tulipata bahati ya kuona kitu ambacho si cha kawaida ktk mazingira ya kila siku. Hii inatokana na kitu kilichofanana na upinde wa mvua kulizunguka jua kwa takriban saa nzima. Wengi tumezoea kuona upinde wa mvua ukichomoza baada ya mvua kubwa kumaliza kunyesha na tena huwa na umbo la upinde unaonzia na kuishia ardhini.

Hii ya leo ilikuwa na umbo la duara ambayo ulilizunguka jua kwa kipindi hicho hali ambayo inatufanya tukose jina sahihi ya kuelezea 'upinde' huu ambao leo ulikuwa duara.

No comments:

Post a Comment