Tuesday, November 16, 2010

maji chumvi na maji 'baridi' yakiwa sambamba - Ras Kutani

Ukiwa umesimama sehemu ya kupatia maakuli iliyopo ktk hotel ya Ras Kutani utapata mandhari mwanana ya mkondo wa maji (lagoon) pamoja na bahari ya hindi vikiwa karibu. Katika picha ya juu, mkondo upo kushoto kwako na kulia kwako ni bahari ya hindi na pwani yake.

'Mlima' wa mchanga unaotenganisha lagoon na bahari.


2 comments:

  1. Hii phenomenon ya "maji baridi" kupishana na "maji chumvi" kwa kilima cha mchanga niliikuta Xai Xai nilipotembelea Mozambique. Pale mikono ya mto Zambezi yanapita upande mmoja na upande wa pili ni maji ya Bahari ya Hindi.

    ReplyDelete
  2. Maji baridi ni maji yasiyo ya bahari au ni maji yasiyo ya chumvi. Hapa kilimanjaro maji katika mito mingi ni mazuri (hayana ladha ya chumvi na magadi) Lakini kuna maeneo ya Same kuna mito ina maji ya magadi. je hawa nitayaita nini? hata mto ruvu nadhani maji yake yana magadi je tutayaita maji baridi?

    ReplyDelete