Monday, September 20, 2010

Oldonyo Lengai

Ni moja ya milima ya volcano ambayo ipo ktk bonde la ufa. Mlima huu upo takriban kilomita 120 toka Mto wa mbu. Ukiwa unatoka Arusha kwenda ngorongoro ufikapo mto wa mbu utakata kona kuelekea upande wa Kulia. Hivi karibuni kulikuwa na tishio la mlipuko toka ktk mlima huo lakini hali ilififia bila ya kutokea mlipuko wenye madhara. Barabara ya kuanzia mto wa Mbu mpaka ulipo mlima huu sio ya lami lakini inapitika na magari kipindi chote.

Wageni wengi wanaoitembelea nchi yetu huja pembezoni ya mlima huu kuuona mlima huu na pia kulitembelea ziwa natron ambalo halipo mbali na mlima huu. Pia pembezoni mwa mlima huu kuna jamii ya wamasai ambao wageni huwatembelea kujifunza maisha yao.
Picha - Tom, Kima Safaris

1 comment:

  1. mwe, blogu zinatoa elimu jamani. Asante sana kwa picha hizi, sikuwahi kuuona mlima huu kwa karibu hivi. Asante mno.

    ReplyDelete