Tuesday, August 3, 2010

Ziwa Momella dogo - Arusha national park

Ziwa momella dogo linavyooneka unavyokuw unalikaribia. Ni moja ya maziwa kadhaa ambayo yapo ndani ya hifadhi ya taifa ya Arusha. Ni moja ya vitu vinavyowavutiwa watu wengi kuitembelea hifadhi hii.

ni Katika ziwa hili la Momella dogo ndipo canoeing (kuendesha mitumbwi) inaruhusiwa kufanywa ktk hifadhi ya Arusha. kwa kuwa ziwa hili lipo ndani ya hifadhi ya taifa, mgeni anayetaka kuendesha mtumbwi ndani ya ziwa hili ni lazima afanye mpango na mwaandaji wake wa safari ili kuweza kupata vibali na uangalizi wakati wa activity hiyo mapema. Canoeing itakuwezesha kusogea karibu na baadhi ya maeneo yaliyopo pembezoni mwa ziwa ambako magari hayafiki na kujionea vizuri vilivyopo huko.

Picha juu ni ukiwa umefika pembezoni mwa ziwa momella dogo. Eneo hili na jingine ambalo lipo upande wa pili wa ziwa hili, wageni wanaruhusiwa kushuka toka ktk magari yao na kutembea. Hapa ni picnic site ambapo mgeni anaweza kupata maakuli yake akiwa ktk mizunguko. Chakula inabidi uwe umekujana nacho. Arusha mjini kuna restaurants kadhaa ambazo wanauza lunch box. Kama umefikia hotel kwa Half/Full board basis basi unaweza fanya mpango ili lunch yako uwekewe kwenye lunch box na iwe tayari mapema unapotoka. Hii ni kwa wale ambao wangependa kufanya safari wenyewe. Kwa wale ambao watakuja kupitia mpango unaosimamiwa na tour company msosi huwa ni sehemu ya package labda kama muandaaji aseme vinginevyo.

Shime wadau, tujifunze na kuzitembelea hizi hifadhi zetu. Kuna mengi ya kujifunza, kufurahisha na hata kuliwaza akili baada ya michakato ya ki-maisha.

No comments:

Post a Comment