Sunday, August 8, 2010

Ni Kilomita 30 toka Arusha

Unakuwa umeshafika ndani ya hifadhi ya taifa ya Arusha kama inavyoonyeshwa hapo juu. Hilo bango unakutana nalo mita chache baada ya kuingia ndani ya hifadhi kupitia geti la Ngongongare. Bango hili pia linakuonyesha muelekeo na umbali wa baadhi ya vivutio vingine vilivyopo ndani ya hifadhi ya Arusha.

Alama hii ipo mita 300 ukiingia ndani ya hifadhi na hapo kuna njia panda. njia ya kulia itakupeleka ilipo makumbusho ya Ngurdoto na hapa utaweza aidha kwenda ngurdoto crater kwenyewe au kuendelea na ruti ya kuelekea yalipo maziwa ya Momella. Ukipita kushoto utapata fursa ya kujionea eneo la wazi lijulikanalo kama Serengeti ndogo na kisha kuweza kuendelea na safari kuelekea geti la Momella. toka hapa mpaka lilipo geti la momella ni kilomita 16. licha ya mwelekeo kuwa tofauti, lakini njia zote zinaweza kukufikisha yalipo maziwa ya momella. njia hizi ni kama mzunguko ambapo zinaweza kukurudisha pale ulipoanzia. kama utaamua kuitembelea hifadhi hii mwenyewe na usafiri wako, basi nunua ramani ufikapo getini ili iweze kukupa mwelekeo wa wapi uende na wapi ulipo.

No comments:

Post a Comment