Wednesday, August 4, 2010

Ngurdoto crater (Rhino point) - Arusha NP

Kwa mujibu wa maelekezo na ramani za njia za ndani ya hifadhi ya Arusha, Rhino point ni eneo ambalo mgeni atakuja kwa lengo la kujionea mandhari ya Ngurdoto crater. Licha ya Rhino point kufikika kirahisi, kwa bahati mbaya crater yenyewe ya Ngurdoto inakuwa haionekani vizuri. Kuna haja ya kufanya mpango wa kuliweka hili sawa. Picha zote ktk mtundiko huu zimepigwa tokea Rhino point moja ya maeneo yaliyotengwa ndani ya hifadhi ya Arusha kwa lengo la kuiangalia Crater ya Ngurdoto ambayo ndio inayoonekana kwenye background.

Miti unayoiona chini ni miti iliyoota kwenye crater ya ngurdoto.

Ngurdoto Crater ikionekana kwenye background kwa off-side.

Kuna sehemu kwa ajili ya wale ambao watapenda kula msosi wao hapa. mabench uyaonayo ni mahususi kwa shughuli hiyo au hata kupumzikia wageni mkiwa hapa. Ngurdoto crater ina view points kadhaa, hii ni mojawapo ambayo siku hii tuliweza kuifikia.

No comments:

Post a Comment