
wa chini na hata wa juu wamekuwa na tabia ya kutumia magari ya wageni kama vantage point. zipo baadhi ya picha ambazo utaona chui yupo juu ya gari la wageni. Hii nayo ni muendelezo wa tabia hii ya kutumia sehemu zilizoinuka (magari) ili kuweza kuona mbali. kwa wa juu au wa chini, kupanda juu ya gari kunampa nafasi ya kuona wapi aelekee ambapo atapata mlo au wapi asipite ili asikutane na sharubu au bwana afya. Siku ukiwa porini na wa juu/wa chini akapanda juu ya gari lako jitahidi uwe mtulivu ili usimshtue. Ni nafasi za nadra sana.
No comments:
Post a Comment