Thursday, July 29, 2010

Pundamilia

Ukweli ni kwamba hakuna pundamilia ambao milia yao inafanana. Milia ni neno lenye kumaanisha hiyo michoro ktk ngozi zao. michoro hii inaweza kufananishwa na alama ktk vidole vya mwanadamu. Sambamba na hilo, kuna aina kadhaa za pundamilia ambao wanapatikana ktk bara la Afrika. Kwa bahati mbaya (ktk mazingira asilia) hapa nyumbani tumebahatika kuwa na aina moja tu ya pundamilia ambao wanajulikana kama Plains Zebra. Aina nyingine zilizopo ni Grevy na Mountain zebras.

Kitu kimoja ambacho kitaweza kukusaidia kutofautisha kati ya plains zebra na aina nyinginezo ni mwendelezo wa milia yao sehemu ya chini ya tumbo. Plains zebra milia yao inafika mpaka sehemu ya chini ya tumbo na kuunganika na milia inayotoka upande mwingine wa mwili. wale wengine, milia yao inakomea juu kidogo kabla ya kufikia chini ya tumbo.

Pata dondoo zaidi za aina hizi tatu za Pundamilia kwa kugonga links zifuatazo: Plains Zebra, Grevy Zebra na Mountain Zebra

Picha zote ni pundamilia wakiwa ndani ya hifadhi ya taifa ya Ruaha; Ahsante ya picha - TTB

No comments:

Post a Comment