Ni barabara ambayo inyoanzia Ngorongoro crater na kukatisha katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti ikielekea maeneo mengine huko kanda ya ziwa. Hivi karibuni Serikali ya Tanzania imesema mpango wa kuijenga barabara hii kufikia kiwango cha Lami umekamilika na kazi inatarajiwa kuanza mwaka 2012. Kauli hii imezua mjadala baina ya makundi mbalimbali kwa jinsi kila moja lilivyoguswa na swala hili. Kikosi cha TembeaTz kiliwahi kupita ktk barabara hii mwaka 2009 kikiwa ktk ziara yake ktk hifadhi za Ngorongoro na Serengeti. Zifuatazo ni baadhi ya taswira za barabara hiyo. Picha juu ni eneo karibu na njia panda ya kueleke Olduvai Gorge. kama unaelekea Serengeti toka Ngorongoro, Olduvai Gorge ipo upande wa kulia wa barabara.
Moja ya agenda kuu inayotolewa na wale wanaopinga ujenzi huu ni kwamba ujenzi huu unaweza athiri (kwa namna moja au nyingine) migration ya wanyama ktk hifadhi ya Serengeti. Picha juu ni kundi la Nyumbu ambalo lilikuwa ni sehemu ya migration likiivuka barabara hii maeneo ya Kusini mwa hifadhi ya Serengeti.
Hapa ni ukiwa unakaribia geti la Naabi (tulikuwa tunatoka Serengeti kurudi Ngorongoro). Mlima uuonao unaitwa naabi na kulifanya geti hili (la kusini mwa Serengeti) kujulikana kama Naabi hill gate.
Inavyoonekana toka juu (picha imepigwa toka ktk hot air balloon). Picha zote ni toka ktk maktaba ya TembeaTz. Bofya hapa kwa habari zaidi hii kama ilivyotundikwa ktk tovuti ya moja ya magazeti ya hapa nyumbani siku kadhaa zilizopita.
No comments:
Post a Comment