Unapokuwa porini na usipokuwa makini mambo mawili yanaweza kukutokea; Unaweza ukakosa kuona baadhi ya vitu adimu vilivyopo huko au ukajikuta upo matatani kwa kuingia sehemu ambazo sizo. Hapa mahali tulipita mwanzo lakini hatukuona kitu cha kutuvutia hivyo tukaendelea kusonga mbele. Baada ya kuendelea mbele na kuona hakuna Dili tukageuza na kurudi sehemu hiyo ktk muda ambao hauzidi hata dk 20. Ndipo tulipogundua ya kuwa mwanzo hatukuwa tukiangalia vyema eneo hilo.
Kulikuwa na Sharubu jike amejibanza kwenye kichaka kilichopo pembezoni mwa mawe hayo. Alikuwa kampumzika hali ambayo iliashiria ya kwamba alikuwa ktk eneo hilo kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment