Licha ya kwamba ni ndege na ana uwezo wa kuruka, Kori Bustard hutumia muda wake mwingi wa siku kutembea ardhini ambako ndiko anakopata chakula chake. Hula zaidi wadudu mbalimbali wanaotambaa ardhini. Huwa anaruka pale tu inapobidi. Majike hutaga mayai yao ardhini pia. Hawajengi viota. Picha ya kwanza ni Kori bustard aliyekutwa Ngorongoro na Mdau Thom wa Kima Safaris wakati picha ya pili ni Kori Bustard akiwa ndani ya hifadhi ya Serengeti ambae timu ya TembeaTz ilikutana nae huko.Kama kuna Mdau mwenye jina la kimatumbi la ndege huyu ruksa kutuhabarisha na kutuelimisha
No comments:
Post a Comment