Picha zifuatazo na kuendelea (chini) ni picha ambazo mdau Thom wa Kimasafaris alizipiga alipokuwa Mikumi mwaka jana. Ni Picha ambazo tofauti yake na picha zilizotangulia ni kwamba hizi zilipigwa kipindi cha ukame. Nadhani tofauti ipo wazi kabisa. Picha juu ni gate kuu la kuingilia ktk hifadhi. Geti hili lipo eneo linalojulikana kama Kikoboga. makao makuu ya hifadhi yapo eno hilo hilo, karibu kabisa na geti hili.


Swala hupenda kuzengea chini ya miti ambako huwa wanakutana na mabaki yanayodondoshwa na ngedere wanapokula matunda ya mtini. Maganda na mabaki wanayodondosha ngedere/nyani ndio huwapa lishe swala hawa.Nia na madhumu ya mitundiko hii (kila hifadhi ina muda wake...) ni kujaribu kukupa hali halisi itakayofanya mdau kufanya safari yako muda muafaka ya kwenda ktk hifadhi. Njia rahisi ya kujua jambo ni kuuliza kwani wahenga walisema mwanzo wa werevu ni kuuliza.....
Unaweza kutembelea tovuti ya TANAPA au Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ambako kuna dondoo zaidi kuhusu muda mzuri wa kutembelea mbuga na sehemu nyinginezo zilizopo ndani ya nchi yetu.
Mtundiko huu umeundwa kwa picha toka kwa Mdau ANM, Thom wa kimsafaris na baadhi toka ktk maktaba ya TembeaTz.
Unaweza kutembelea tovuti ya TANAPA au Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ambako kuna dondoo zaidi kuhusu muda mzuri wa kutembelea mbuga na sehemu nyinginezo zilizopo ndani ya nchi yetu.


No comments:
Post a Comment