Thursday, May 13, 2010

Iko shida; Mikumi

Ngiri amepewa jina la iko shida kwa tabia yake ya kukimbia umbali fulani na kisha kusimama na kugeuka nyuma kama vile anawauliza wanaomkimbiza au kumshtua kama kuna shida yoyote. Mdau mmoja alitanabaisha ya kuwa ngiri anakuwa na tabia hii kutokana na kuwa na uwezo mdogo wa kukumbuka mambo. Anaposhtuliwa ataanza kutimua mbio kama ilivyo ada kwa kiumbe hai yoyote yule, muda si mrefu atasahau kitu kilichomfanya aanze kutimua mbio. Akigundua hivyo, atasimama na kuangalia nyuma (kule alipokuwa anatoka) ili aweze kukumbuka ni kitu gani kilimfanya aanze kutimua mbio.

Ndio maana ukiwa porini hawa jamaa utawakuta muda mwingi wanakuwa wanakimbia ovyo ovyo bila ya sababu ya msingi. nadhani mtundiko huu utakupa mwangaza juu ya tabia hii aliyonayo ngiri. Picha zote ni hifadhi ya Taifa ya mikumi na shukran ya picha kwa mdau ANM.

No comments:

Post a Comment