Saturday, April 3, 2010

Mandhari: Marangu gate - Mandara hut.... Kilimanjaro

Hivi ndivyo libeneke la kukwea mlima kilimanjaro linavyoanza. Baada ya kupita Marangu Gate safari huanza kwa timu (Mpandaji + Guide + Porters) kuelekea Mandara hut (2700m ASL). Sehemu kubwa ya safari inakuwa ni kwenye msitu kama inavyoonekana. Hii ndio Marangu route yenyewe.

mkiwa njiani mnakutana na mandhari nzuri za mito.


Wamekimbia mijini wameenda kujichimbia milimani. mwisho wa siku zao ni kuzengea mabaki. kama wangekuwa na manufaa kwa jamii, nadhani wangekuwa wameshaingizwa ktk list ya viumbe walio ktk hatihati ya kutoweka duniani. hapo ni ktk moja ya picnick/lunch point mkiwa njiani.

hizi ndio njia wanazopita wapandaji wanaotumia Marangu route. Msitu huu ni sehemu ya Kilimanjaro National park. Huku hakuna wanyama wakali. Mbega ndio wanaopatikana kwa sana.

Picha: Mdau

No comments:

Post a Comment