Saturday, March 27, 2010

Taswira maridhawa - Lake Manyara

Njia unayoiona ni njia inayoanzia Makuyuni, kupitia mto wa Mbu, Karatu, Ngorongoro mpaka Serengeti. Ni njia muhimu kwani inaunganisha vivutio vingi vilivyopo kanda ya kaskazini. lami unakuwa unatoka nayo Arusha mpaka unapoingia NCAA - Ngorongoro Conservation Area Authority.
Licha ya kukuonyesha msitu wa Lake manyara national park, taswira hii pia inakuonyesha mandhari ya bonde la ufa. Mteremko mkali unaouona kulia ni kingo za Bonde la ufa. Picha imepigwa tokea pembezoni mwa bwawa la kuogelea la Lake Manyara Serena lodge.

No comments:

Post a Comment