Thursday, January 7, 2010

Huo sio mwayo...


Unaweza ukadhani viboko hawa ndio wametoka kuamka na wanajinyoosha kama vile ambavyo sisi binadamu tufanyavyo baada ya mapumziko. Si kweli

Hiyo ni ishara kwako au kiboko mwenzie kwamba anaingia ktk himaya ambayo hatakiwi. Kiboko hufanya hivyo ili kutoa onyo kwa yoyote yule ambae anaingia ktk eneo lake. Kiboko Dume humiliki bwawa au eneo ndani ya bwawa. Hulimiliki eneo hilo sambamba na majike yaliopo ktk eneo lake. Ktk hilo bwawa au eneo ndani ya bwawa, kiboko mwingine dume hatakiwa kusogea. akiingia kwenye 18 basi hapo lazima pachimbike. hiyo warning huitwa the giant gape.

[Shukran kwa picha: Antelope Safaris]

No comments:

Post a Comment