Monday, September 7, 2009

Kwanini Wanyama wa Serengeti wanahama??

Nyumbu wakihama toka sehemu moja kwenda nyingine ktk Mbuga ya Serengeti

Nyumbu, Pundamilia na swala huwa wanahama toka sehemu moja ya Serengeti na kwenda sehemu nyingine na mara nyingine hata kufika ktk mbuga ya Masai Mara.
Sababu kuu za uhamaji wao ni mbili; Malisho mazuri na Usalama wao.

Wanyama hawa huwa wanapenda kula nyasi ndogo ndogo (zile zinazoanza kuchipua). hawapendi kula nyasi ndefu. Nyasi zinapokuwa ndefu zinahatarisha usalama wa wanyama hawa. nyasi ndefu huwa ni maficho mazuri kwa simba na wanyama wengine wala nyama.

1 comment:

  1. na kwasababu hiyo ya usalama uliyoitaja, majike wa wanyama hawa hubeba mimba wanapokaribia kuhama hivyo huzaa watoto wao wakiwa kwenye usalama na wakati wanarudi tayari watoto wanakuwa wamepata nguvu angalau ya kuweza kujikinga na adui kama kukimbia nk.

    ReplyDelete