Monday, November 30, 2009

Dont Try this at Home!

meserani snake park, Arusha



Kila mara niwapo Arusha na ninapopata nafasi huwa najikuta naenda Messerani snake park kuangalia na hasa hasa kuchezea baadhi ya nyoka wanaofugwa hapo.
Mwanzoni uwoga ulitawala, lakini hii kitu ni kama kula nyama ya mtu. ukianza ndio basi, uoga unapotea.

Nyoka huyo niliambiwa ni Home-stead snake, hana sumu na yeye huua kwa kutumia msuli (constrictor) kama chatu. hii ilikuwa ni December 2008.

Hippo Camp, Selous game reserve

Hippo Camp ni moja ya makambi ya kufikia wageni wanaotembelea mbuga ya Selous. Kambi hii ipo nje ya mbuga ktk kijiji cha Mloka, Pembezoni kabisa mwa Mto Rufiji kama unavyojionea hapo juu.

Sehemu ya Kuegeshea na kupanda boat kwa ajili ya Boat ride

Off-course, you cant have a hippo camp near Rufiji without the Hippo themselves. Hippopotamus ndani ya Mto Rufiji, mbele ya Hippo camp

Bwana Afya

Fisi, Serengeti


kwa mbali ni uwanja wa ndege wa Seronera.

Mandhari maridhawa ktk milima ya kitonga




picha hizi nilizipiga 26th Nov 2009; ni mandhari maridhawa ktk mlima Kitonga

Tembea ujionee maajabu

nguzo zikiwa upande wa kushoto mwa barabara ukiwa unatokea Makambako.

Nyaya za umeme zikahamia upande wa kulia (nguzo ya pili mbele utaona nyaya zinahamia upande wa kulia wa Barabara)
makaburi chini ya mti, nyaya zikiwa upande wa Kulia wa barabara
------------------------------------------

Ukiwa unasafiri kutoka Makambako kuja Iringa mjini, utapita eneo linaloitwa Tanangozi. Moja ya mambo ambayo hustaajabisha wengi wanaosafiri ktk barabara hii ni kuhama ghafla kwa nguzo za umeme (I'm sure ni za Tanesco) toka upande mmoja wa barabara na kurudi upande wake wa awali ktk umbali mfupi tu!

Niliwahi sikia hizi habari lakini hivi majuzi nilipata bahati ya kujionea mwenyewe hali hii. Mengi yanaweza kusemwa lakini kikubwa kinachoelezewa ni kwamba;
Nyaya za Umeme zilipopita juu ya makaburi , umeme ukawa hauwezi kupita- nikimanisha toka kule unapotoka hadi kueleka kule unapotakiwa kwenda destination.
baada ya mafundi kuhangaika sana wakagundua kuwa umeme 'unapotea' nguzo moja kabla ya nyaya zao kupita juu ya hayo makaburi. Baada ya majadiliano na consultation, timu ilikubaliana kuwa ili kuweza kukamilisha kazi, nyaya hizo zivushwe upande wa pili wa barabara ili zisipite juu ya makaburi na kuwezesha umeme kupita kama inavyotakikana. na mita kadhaa baada ya makaburi, nyaya zikarudishwa upande wake wa awali wa barabara ili kuweza kuendelea na safari.

Tembea uone...

Friday, November 20, 2009

Birds Fascinate me!

Jina lake limenitoka, Selous

Secretary bird, Serengeti

Eagle, Serengeti


Jina lake limenitoka pia, Serena - Serengeti

Jina limenitoka, selous

Flamingo, dsm zoo



Picha za wanyama au ndege wa porini mara nyingi huwa hazihitaji maelezo; huwa zinajieleza zenyewe; labda kama kunakuwa na tukio muhimu. Unapokuwa porini, nyakati nyingine unaweza kuona kitu fulani ni cha kawaida ukakiacha. baada ya kurudi camp unagundua kuwa ume-miss kugandisha kitu kizuri. wakati mwingine unapiga picha huku ukisema "hii picha sio kali..." lakini ukija kui-export ktk laptop na kuiangalia baadae, inakuwa inaleta hisia tofauti sana.

kifupi, naamini hata kama kunguru wangekuwepo porini, picha ya kunguru wa porini ingekuwa na mvuto wa kipekee tofauti na ya kunguru aliye mjini.

Picha juu ni picha za ndege mbalimbali ambazo niliwahi kuzigandisha ktk mizunguko yangu porini. zina ujumbe na hisia nzito. Wengine majina yao magumu na kwa sasa yamenitoka

for bird watchers, dedication kwenu........
KK

Mtalii ni nani??

nani anastahili kuitwa mtalii? ni mambo yepi mtu anatakiwa kuyafanya ili aitwe mtalii na sio msafiri?
Uraia wa mtu unahusika vipi na mtu kuwa mtalii au sio mtalii?
Uwepo wa mtu katika eneo fulani kunakufanya wewe kuwa mtalii?

Thursday, November 5, 2009

Golini




Kama umewahi kusafiri kwa gari kutoka ngorongoro kwenda serengeti, basi lazima utakuwa umepita sehemu hii ambayo ni maarufu kama 'Golini'. hapo ndio mwisho wa Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) na mwanzo wa Serengeti National park.